Uchaguzi huo haufanyiki katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo ambayo yana mzozo na jimbo jirani la Puntland. Tangu ilipojitangazia uhuru wake kutoka kwa Somalia mwaka 1991, Somaliland imekuwa ikipata mafanikio taratibu , lakini thabiti kuelekea demokrasia.Inaripotiwa kuwa watu wengi wamejitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo na kuna misururu mirefu nje ya vituo vya kupigia kura Hadi uchaguzi huu, ni vyama vitatu vilivyo ruhusiwa kuendesha shughuli zake . Sasa mfumo umewekwa na vyama saba vinachuana katika uchaguzi wa mitaa .
No comments:
Post a Comment