Rais Barack Obama, katika muhula wake wa kwanza, alizuru Afrika mara moja tu, tena kama mpita njia, na kusema wazi kwamba hangekuwa anajihusisha kupita kiasi na maswala ya Afrika. Kwa hivyo, ni mabadiliko yapi yatakayokuwepo katika muhula wa pili?“Hatima ya Afrika iko mikononi mwa Waafrika wenyewe,” alisema huko Ghana, katika hotuba iliyodhihirisha wazi kwamba ushawishi wa Marekani unapungua katika bara ambalo sasa linafanya biashara zaidi na Uchina kuliko Marekani. “Kama Kenya itafanya uchaguzi huru, basi Obama ataitembelea nchi hiyo. ''Swala hili la yeye kutokuwa na muda na Afrika, kwa sababu ya matukio mengine, halikutiwa mkazo katika uchaguzi ulioangazia maswala nyeti nchini Marekani na harakati za mapinduzi katika nchi za Kiarabu. Akitoa hotuba yake baada ya kushinda, Bwana Obama aligusia tu “,muongo wa vita” na “watu walioko katika nchi za mbali… wanaoweka maisha yao hatarini ili tu kujadili masuala muhimu, na kupata nafasi, kama sisi, kupiga kura kama sisi tulivyopiga leo”
No comments:
Post a Comment