| BofyaYahya Toure.Mcheza kiungo kutoka Ivory Coast, anayeichezea Manchester City ya Uingereza. Toure aliiongoza Manchestert City kushinda kombe la ligi kuu ya Premier ya England kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 44 iliyopita. |
| BofyaDemba Ba kwa sasa ni mmoja wa wachezaji nyota wa klabu ya Newcastle na kufikia sasa tayari amefunga jumla ya magoli 6 katika ligi kuu ya premier la England na anatarajiwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Senegal kitakachocheza katika fainali ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika. |
| BofyaDidier Drogba ni noadha wa timu ya taifa ya Ivory Coast, amewahi kuongoza Chelsea kushinda kombe la ligi kuu ya Premier ya England pamoja na kombe la klabu bingwa barani ulaya. |
| BofyaChristopher Katongo ni mchezaji wa timu ya taifa ya Zambia maarufu kama Chipolopolo na aliiongoza timu hiyo kushinda fainali ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika |
| BofyaYounes Belhanda ni mchezaji mwenye umri wa miaka 22, na mmoja wa wachezaji waliotia fora na kuisaidia klabu ya Montepellier, kushinda kombe la ligi kuu kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya karne moja tangu klabu hiyo ilipobuniwa. |
No comments:
Post a Comment