Wednesday, November 28, 2012

MISRI WATU WAKESHA KUMPINGA RAIS MURSI.


Walikesha wakiimba nyimbo za kumlaani rais pamoja na vuguvugu lake la kiislamu la Muslim Brotherhood. Maandamano mengine ya kumpinga rais Morsi yamefanyika katika maeneo mbali mbali nchini humo.Jana Jumanne, maelfu ya waandamanaji walifurika katika medani hiyo wakiandaa mandamano kadhaa huku wakisema watamkiuka rais Mursi huku wakipinga mamlaka aliyojilimbikizia. Bwana Morsi amejaribu kumaliza mzozo huo kwa kuahidi kuwa madaraka yake yatakuwa na kikomo.

No comments:

Post a Comment