Hasira dhidi ya filamu hiyo iliyokuwa inamkejeli Mtume Mohammed, ilisababisha maandamano dhidi ya Marekani kiasi cha kuteketezwa ubalozi wake nchini Libya. Hukumu hizo ziliidhinishwa na Mufti mkuu nchini Misri ambaye pia ni msomi wa dini ya kiisilamu.Washukiwa hao saba walihukumiwa wakiwa hawapo mahakamani.Filamu hiyo iliyokuwa ya hali ya chini mno, ilitengezwa mjini Carlifonia, Marekani na kutolewa kwenye internet mwezi Septemba. Miongoni mwa wale walioshtakiwa ni mtengezaji wa filamu yenyewe Morris Sadek ambaye ni raia wa Misri. Mahakama itatoa hukumu ya mwisho mwezi Januari kufuatia itikio la Mufti.
No comments:
Post a Comment