Monday, December 31, 2012

MATOKEO YA SENSA IDADI YA WATU TANZANIA 2012

JUMLA TUKO 44,929,002 TANZANIA BARA 43,625,434 ZANZIBAR 1,303,568

Thursday, December 13, 2012

UPINZANI KUPIGA KURA YA "HAPANA" MISRI


Awali upinzani uliwataka wafuasi wake kuisusia kura ya maoni ikisema kuwa katiba mpya inawanyima watu faida za mapinduzi ya kiraia yaliyofanyika nchini humo na kumwondoa mamlakani aliyekuwa rais Hosni Mubarak. Lakini Hamdeen Sabahi, mmoja wa viongozi wa upinzani, alisema kuwa watashiriki tu katika kura ya maoni ikiwa majaji pamoja na waangalizi wa kimataifa watakubali kuendesha mchakato huo.Wamisri walio ugenini wameanza kuipigia kura katiba hiyo mpya baada ya balozi za nchi hiyo ugenini kuanza rasmi shughuli hiyo. Mazungumzo ya kupatanisha pande zinazovutana kuhusu katiba mpya, ambayo yalipaswa kuandaliwa leo, yaliakhirishwa. Mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema kuwa serikali inatuma ujumbe unaogongana kuhusu siku ambayo upigaji kura utakamilika.

Wednesday, December 12, 2012

TANZANIA GETS 489.9 MILLION LOAN TO FIGHT POVERTY.

The government has signed a loan agreement worth 489.9m/- with the World Bank to support its efforts of enhancing country's economic growth and poverty reduction.

UPINZANI KUPINGA RASMI MATOKEO YA UCHAGUZI GHANA


Chama cha upinzani NPP kimesema kuwa kitakwenda mahakamani kupinga uhalali wa Rais John Mahama. Pia kinasema kuwa kitasusia vikao vya bunge. Ushindi huu ulimtosheleza kuweza kukwepa duru ya pili dhidi ya mpinzani wake Nana Akufo-Addo aliyepata asilimia arobaini na saba ya kura.Mnamo siku ya Jumapili, tume ya uchaguzi ilimtangaza bwana Mahama kama mshindi wa uchaguzi huo kwa kushinda kwa asilimia hamsini na saba. Waangalizi kwenye uchaguzi huo wanasema kuwa ulikuwa huru na wa haki. Ghana imekuwa ikitolewa kama mfano wa nchi iliyokomaa kidemokrasia katika bara la Afrika.

MISRI MAANDAMO YAENDELEA.


Wanajeshi wanashika doria kwa kutumia vifaru huku wakiwa wameweka vizuizi vya seng'enge na matofali, nje ya ikulu ya rais Mohammed Morsi. Wafuasi wa bwana Morsi wameitisha maandamano yao kufanyika sambamba na yale ya upinzani.Makundi ya upinzani yanataka afutulie mbali kura ya maoni iliyopangwa kufayika siku ya Jumamosi juu ya katiba hiyo mpya. Rais Morsi anasema kuwa katiba mpya italinda faida zilizotokana na mapinduzi ya kiiraia yaliyomwondoa mamlakani rais Hosni Mubarak mwaka jana, lakini wapinzani wake wanasema anarejesha nchi nyuma, katika mizizi ya kidikteta. Siku ya Jumatatu, kulikuwa na taarifa za ghasia na vurugu mjini Cairo, huku wapinzani waliokuwa wamekesha katika medani ya Tahrir wakifyatuliwa risasi.

Monday, December 10, 2012

RIO FERDINAND HIT IN THE EYE

Manchester United defender Rio Ferdinand was hit in the head by a two-pence coin thought to be thrown from the crowd as his team's derby clash with Manchester City ended in an ugly clash this afternoon (pictured left). Ferdinand was seen wiping blood from his face following the incident (right) which took place in the aftermath of United's injury-time winning goal in their 3-2 victory at the Etihad Stadium.

MANDELA ALAZWA HOSPITALINI SIKU YA 2.


Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amelezwa hospitali kwa siku ya pili mjini Pretoria ambako alipelekwa Jumamosi. Maafisa wamesema kwamba amekuwa akifanyiwa uchunguzi, ingawaje haijajulikana kwamba ni uchunguzi wa aina gani.

JOHN MAHAMA ASHINDA UCHAGUZI GHANA.


 Bwana Mahama alishinda kwa asilimia 50.7 dhidi ya mpinzani wake Nana Akufo-Addo aliyepata 47.74%. Rais Mahama aliwasihi "viongozi wote wa vyama vyote vya kisiasa kuheshimu uamuzi wa wananchi".Hata hivyo chama cha upinzani cha NPP kimesema kwamba kitayapinga matokeo hayo, huku kikilaumu chama tawala cha NDC kwa kupanga njama na tume hiyo ili kubadilisha matokeo ya uchaguzi uliofanyika Ijumaa. "Sauti ya wananchi ni sauti ya Mungu," alisema. Polisi mjini Accra walilazimika kufyatua vitoa machozi ili kuwatawanya wafuasi wa upinzani waliokuwa wamekusanyika nje ya ofisi za tume hiyo. Wakati matokeo yakitangazwa, vifaru vilikuwa vikilinda ofisi za tume hiyo, na barabara zilizoizunguka zilikuwa zimewekwa vizingiti na polisi. "Mabibi na mabwana, kulingana na matokeo tuliyopata, namtangaza John Dramani Mahama kama rais-mteule," mkuu wa tume Kwadwo Afari-Gyan aliwaambia waandishi habari.BwAlisema asilimia 80 ya wapigaji kura walijitokeza.

RAIS KIKWETE ATUNUKU NISHANI IKULU


BONDIA FRANCIS MIYEYUSHO ASHINDA.

BONDIA FRANCIS ASHINDA ROUND 10 K.O.


XXL AFTER SCHOOL BASH 2012






Friday, December 7, 2012

OBAMA TURNS ON THE LIGHTS AT THE CAPITOL

The Obamas were joined by actor Neil Patrick Harris to help light the National Christmas Tree in the 90th annual ceremony. All were bundled to shield themselves from the cold December night. After the tree was lit, the first family even partook in some holiday caroling, with Mr Obama and daughter Malia singing 'Santa Claus Is Coming to Town.'

SCARRED FOR LIFE

Many migrants in Greece face daily racist attacks, police apathy and a system that punishes them rather than their assailants. Hassan Mekki, a 32-year-old Sudanese migrant who fled conflict in his country in hope of a better life in Europe - has been left fearing for his life after he was attacked by a group of men on motorcyles. They left large gashes resembling an 'X' across his back.

JESHI LAWAONDOA WAANDAMANAJI MISRI


Limetuma vifaru na magari mengine yaliyo hamiwa kwa silaha nje ya kasri la rais baada ya mapigano ya usiku kucha kati ya wafuasi na wapinzani wa rais Mohammed Morsi. Makabiliano yamesababisha vifo vya watu watano na wengine zaidi ya mia sita wakijeruhiwa.Walioshuhudia matukio wanasema kuwa waandamanaji wameanza kuondoka kutoka eneo hilo. Taarifa za televisheini ya taifa zinasema kuwa rais Morsi atatoa hutuba kwa taifa baadaye leo. Mamlaka kuu ya waisilamu, Al-Azhar,imemtaka rais kufutilia mbali mamlaka aliyojilimbikizia. Viongozi wa upinzani wameitisha maandamano zaidi hii leo kupinga hatua ya rais kujipa mamlaka zaidi pamoja na kuipinga rasimu ya katiba mpya inayotarajiwa kupigiwa kura tarehe 15 mwezi huu.

Thursday, December 6, 2012

KIKWETE AZINDUA WODI YA WAZAZI LINDI



RAIS KIKWETE AZINDUA WODI YA WAZAZI KINYONGWA KILWA, AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA PIA AKAGUA MAABARA KATIKA SHULE YA MITOLE.

WATU 270 WAFARIKI DUNIA KATIKA KIMBUNGA FILIPINO



Wengine wengi hawajulikani waliko. Nusu ya walioathiriwa walikuwa ni wakaazi katika maeneo ya milima walioathirika na maporomoka ya udongo baada ya kuyakimbia makaazi yao ili kwenda kwenye maeneo yalio salama. Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la AP Miili zaidi ya 270 ya watu waliofariki katika kimbunga hicho ilipokelewa katika maeneo yalioathiriwa na kimbunga hicho kusini mwa ufilipino.Katibu mkuu wa shirika la msalaba mwekundu nchini humo, Gwendolin Paang, ameiambia BBC kuwa idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka. Kwa mujibu wa maafisa nchini humo huenda miili zaidi ikapatikana katika maeneo mengine ambayo kwa sasa waokoaji wanaendeleza shughuli za uokozi.

Wednesday, December 5, 2012

WAANDAMANAJI WAZINGIRA IKULU MISRI


Wafuasi wa rais huyo wameharibu mahema yaliyowekwa nje ya ikulu hiyo na wapinzani wa Morsi walioanza kukesha nje ya ikulu hiyo Jumanne kupinga mamlaka aliyojilimbikizia. Makamu wa rais Mahmoud Mekky,amesema kuwa mabadiliko yaliyofanyiwa katiba hiyo yanaweza kukubalika na upinzani.Pia wanapinga rasimu ya katiba mpya ambayo itapigiwa kura ya maoni tarehe 15 mwezi Disemba. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani,Hillary Clinton amesema mazungumzo yanahitajika haraka kuhusu katiba hiyo. Maelfu ya wapinzani wa rais wameapa kuendelea na maandamano yao nje ya ikulu ya rais mjini Cairo. Baadhi wameweka mahema nje ya ikulu na sasa wanuzunguka ukuta wa ikulu hiyo. Siku ya Jumanne , maelfu ya waandamanaji walivamia ikulu wakipinga rasimu ya katiba iliyozua utata mkubwa pamoja na kupinga sheria inayomlimbikizia mamlaka makuu Rais Morsi.              

Monday, December 3, 2012

MOURINHO COULD REPLACE SIR ALEX AT MANCHESTER UNITED


Sir Alex Ferguson believes Jose Mourinho could be the man to replace him at Manchester United. A fortnight ago the pair shared afternoon tea at the Lowry Hotel.

GOODBYE AMERICA BECKHAM FINISHED CAREER IN USA


MORE WOMEN BEHID THE WHEEL

Between 1995 and 2010 the number of women with a driving licence grew by 23 per cent, a rise of 2.6million to 13.8million.

FACEBOOK TO BUY WHATSAPP

Facebook is reportedly in talks to acquire mobile chat program Whatsapp, according to TechCrunch. The news comes from “sources close to the matter”, but there are no specific details on the price and stage of the deal. Whatsapp is prominent among mobile users, with over 1 billion messages a day sent on the multi-platform chat service.
Whatsapp is also available on BlackBerry, Symbian, and Windows Phone.

MAJAJI KUSUSIA KURA YA MAONI MISRI



Taarifa hiyo ya muungano huo wa mahakimu, inajiri baada ya kuwepo mvutano kati ya mahakama ya juu nchini Misri na wafuasi wa rais Morsi wenye itikadi kali za dini ya kiislamu.Upinzani unasema rasimu inashusha hadhi ya uhuru wa watu.Mahakama ya kikatiba imetangaza kuwa inasitisha shughuli zake kwa muda usiojulikana baada ya mahakimu wa mahakama hiyo kuzuiwa kutoa uamuzi kuhusu uhalali wa baraza rasimu hiyo ya katiba.

KENYATTA NA RUTO WAUNGANA RASMI KUGOMBEA URAIS


Katika mkutano wa hadhara uliofanywa mjini Nakuru makamo wa Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta, alisema atagombea urais na waziri wa zamani, William Ruto, alisema yeye atakuwa mgombea mwenza wa Bwana Kenyatta. Siku ya Ijumaa shirika la Kenya la kutetea haki (the International Centre for Peace and Conflict) lilifikisha kesi mahakama makuu kudai kuwa wanasiasa hao hawafai kushika madaraka. Wanasiasa wengine maarufu wa Kenya piya wameshtakiwa na ICC.