Awali upinzani uliwataka wafuasi wake kuisusia kura ya maoni ikisema kuwa katiba mpya inawanyima watu faida za mapinduzi ya kiraia yaliyofanyika nchini humo na kumwondoa mamlakani aliyekuwa rais Hosni Mubarak. Lakini Hamdeen Sabahi, mmoja wa viongozi wa upinzani, alisema kuwa watashiriki tu katika kura ya maoni ikiwa majaji pamoja na waangalizi wa kimataifa watakubali kuendesha mchakato huo.Wamisri walio ugenini wameanza kuipigia kura katiba hiyo mpya baada ya balozi za nchi hiyo ugenini kuanza rasmi shughuli hiyo. Mazungumzo ya kupatanisha pande zinazovutana kuhusu katiba mpya, ambayo yalipaswa kuandaliwa leo, yaliakhirishwa. Mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema kuwa serikali inatuma ujumbe unaogongana kuhusu siku ambayo upigaji kura utakamilika.
No comments:
Post a Comment