Friday, December 7, 2012

JESHI LAWAONDOA WAANDAMANAJI MISRI


Limetuma vifaru na magari mengine yaliyo hamiwa kwa silaha nje ya kasri la rais baada ya mapigano ya usiku kucha kati ya wafuasi na wapinzani wa rais Mohammed Morsi. Makabiliano yamesababisha vifo vya watu watano na wengine zaidi ya mia sita wakijeruhiwa.Walioshuhudia matukio wanasema kuwa waandamanaji wameanza kuondoka kutoka eneo hilo. Taarifa za televisheini ya taifa zinasema kuwa rais Morsi atatoa hutuba kwa taifa baadaye leo. Mamlaka kuu ya waisilamu, Al-Azhar,imemtaka rais kufutilia mbali mamlaka aliyojilimbikizia. Viongozi wa upinzani wameitisha maandamano zaidi hii leo kupinga hatua ya rais kujipa mamlaka zaidi pamoja na kuipinga rasimu ya katiba mpya inayotarajiwa kupigiwa kura tarehe 15 mwezi huu.

No comments:

Post a Comment