Wednesday, December 12, 2012

UPINZANI KUPINGA RASMI MATOKEO YA UCHAGUZI GHANA


Chama cha upinzani NPP kimesema kuwa kitakwenda mahakamani kupinga uhalali wa Rais John Mahama. Pia kinasema kuwa kitasusia vikao vya bunge. Ushindi huu ulimtosheleza kuweza kukwepa duru ya pili dhidi ya mpinzani wake Nana Akufo-Addo aliyepata asilimia arobaini na saba ya kura.Mnamo siku ya Jumapili, tume ya uchaguzi ilimtangaza bwana Mahama kama mshindi wa uchaguzi huo kwa kushinda kwa asilimia hamsini na saba. Waangalizi kwenye uchaguzi huo wanasema kuwa ulikuwa huru na wa haki. Ghana imekuwa ikitolewa kama mfano wa nchi iliyokomaa kidemokrasia katika bara la Afrika.

No comments:

Post a Comment