Wafuasi wa rais huyo wameharibu mahema yaliyowekwa nje ya ikulu hiyo na wapinzani wa Morsi walioanza kukesha nje ya ikulu hiyo Jumanne kupinga mamlaka aliyojilimbikizia. Makamu wa rais Mahmoud Mekky,amesema kuwa mabadiliko yaliyofanyiwa katiba hiyo yanaweza kukubalika na upinzani.Pia wanapinga rasimu ya katiba mpya ambayo itapigiwa kura ya maoni tarehe 15 mwezi Disemba. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani,Hillary Clinton amesema mazungumzo yanahitajika haraka kuhusu katiba hiyo. Maelfu ya wapinzani wa rais wameapa kuendelea na maandamano yao nje ya ikulu ya rais mjini Cairo. Baadhi wameweka mahema nje ya ikulu na sasa wanuzunguka ukuta wa ikulu hiyo. Siku ya Jumanne , maelfu ya waandamanaji walivamia ikulu wakipinga rasimu ya katiba iliyozua utata mkubwa pamoja na kupinga sheria inayomlimbikizia mamlaka makuu Rais Morsi.
No comments:
Post a Comment