Wengine wengi hawajulikani waliko. Nusu ya walioathiriwa walikuwa ni wakaazi katika maeneo ya milima walioathirika na maporomoka ya udongo baada ya kuyakimbia makaazi yao ili kwenda kwenye maeneo yalio salama. Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la AP Miili zaidi ya 270 ya watu waliofariki katika kimbunga hicho ilipokelewa katika maeneo yalioathiriwa na kimbunga hicho kusini mwa ufilipino.Katibu mkuu wa shirika la msalaba mwekundu nchini humo, Gwendolin Paang, ameiambia BBC kuwa idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka. Kwa mujibu wa maafisa nchini humo huenda miili zaidi ikapatikana katika maeneo mengine ambayo kwa sasa waokoaji wanaendeleza shughuli za uokozi.
No comments:
Post a Comment