Monday, December 10, 2012

JOHN MAHAMA ASHINDA UCHAGUZI GHANA.


 Bwana Mahama alishinda kwa asilimia 50.7 dhidi ya mpinzani wake Nana Akufo-Addo aliyepata 47.74%. Rais Mahama aliwasihi "viongozi wote wa vyama vyote vya kisiasa kuheshimu uamuzi wa wananchi".Hata hivyo chama cha upinzani cha NPP kimesema kwamba kitayapinga matokeo hayo, huku kikilaumu chama tawala cha NDC kwa kupanga njama na tume hiyo ili kubadilisha matokeo ya uchaguzi uliofanyika Ijumaa. "Sauti ya wananchi ni sauti ya Mungu," alisema. Polisi mjini Accra walilazimika kufyatua vitoa machozi ili kuwatawanya wafuasi wa upinzani waliokuwa wamekusanyika nje ya ofisi za tume hiyo. Wakati matokeo yakitangazwa, vifaru vilikuwa vikilinda ofisi za tume hiyo, na barabara zilizoizunguka zilikuwa zimewekwa vizingiti na polisi. "Mabibi na mabwana, kulingana na matokeo tuliyopata, namtangaza John Dramani Mahama kama rais-mteule," mkuu wa tume Kwadwo Afari-Gyan aliwaambia waandishi habari.BwAlisema asilimia 80 ya wapigaji kura walijitokeza.

No comments:

Post a Comment